MAISHA ONLINE BLOG

Hot

Post Top Ad

LightBlog

Post Top Ad

Your Ad Spot

Sunday, April 8, 2018

PADRI MWINGINE WA KANISA KATOLIKI AUAWA KWA RISASI

11:23:00 PM 0
Kasisi wa kanisa katoliki amepigwa risasi na kufa Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemkrasia ya Kongo.

Vyanzo vya habari kutoka Kaskazini mwa jimbo la Kivu vimearifu kuwa Padri Étienne Nsengiunva alikuwa akikomnisha waumini na ndipo wakati mtu mwenye silaha alipoingia kanisani na kumpiga risasi.
Tukio hilo lilijiri wakati wa sherehe za ibada ya ubatizo wa wakristo wapya na wanandoa wapya.
Taarifa zinadai kuwa muuaji huyo ni kutoka katika kundi la waasi wa Mai Mai Nyatura ambalo ni miongoni mwa vikundi vinavyopambana kudhibiti jimbo hilo lenye rasilimali za madini lakini pia uporaji wa fedha kutoka kwa wanavijiji
Read More

Saturday, October 7, 2017

MAISHA ONLINE BLOG: SIMULIZI LA KWELI: WEMA HAUOZI

SIMULIZI LA KWELI: WEMA HAUOZI

11:56:00 AM 0

SIMULIZI LA WEMA HAUOZI

Nakumbuka ilikuwa ya pata miaka mingi iliyopita ambapoa nililazimika kufunga safari kuelekea mkoani katavi Mkoa ambao naweza sema kwangu mimi ulikua ni mkoa wa ahadi.
Nililazimika kwenda mara baada ya kumaliza chuo cha upapalazi na huko ndiko ambapo kulikuwa na nafasi ya ajira , hivyo miongoni mwa watu wengi ambao waliomba nafasi ya kazi kwenye kituo kimoja cha upapalazi. Nami nilikuwemo.
Katika safari yangu nakumbuka nilikua nimepanda Basi kampuni ya AMC nilikua natoka Tabora kuelekea mkoani katavi. Sauti ya konda ilisikika ikisema tutatumia dakika kumi  tu kunywa  chai na kuchimba dawa. Nilistuka kwani  kausingingizi kalikuwa kamenipitia japo miaka hiyo ilikuwa ni ngumu sana kupata usingizi kama umepanda  Basikwa barabara ya TABORA  via KATAVI. Maana njia ilikuwa si njia  mabonde si mabonde na mashimo barabara nzima.
Kwaharaka haraka kuhofia muda niliagiza chakula  na nikaka kwenye meza moja ambayo ilikua na viti vitatu lakini havikuwa na mtu ni mimi tu ndo nilikuwa hapo  ingawaje pembeni yangu kulikuwa na meza ambayo siti zilipambwa na familia ya baba na mama na mtoto mmoja walioonekana ni wenye furaha na walikuwa wakipata chakula pamoja na vinywaji.
Basi nikaendelea kunywa na mara nilipo maliza nikaenda kaunta ya chakula ilinilipe naingiza mfuko mara sioni pesa , pesa ambayo nakumbuka ilikuwa nikiasi kidogo tu ambacho nilikikusanya kwa chasho la kuuza mchicha, tena nakumbuka kipindi ambacho niko nyumbani tulianzisha bustani ya mbogamboga kukidhi haja ya mahitaji madogomadogo . wakati mimi nikitumia nguvu kubwa kuikusanya pesa hiyo iliniweze pata nauri ya kunipeleka kwenye ahadi  ya ngu mpaya. Yaani mkoani Katavi kwenye Usahiri.
Heee kilicho tokea sikuamini baada ya kumwambia mhudumu kuwa siioni pesa nilikuwa na pesa mfukoni ssa siioni, ndugu. Niliporomoshewa matusi ambayo sijawahi hata yasikia tangu utoto wangu, huku Boss wa eneo hilo akisema vijana wasiku hizi bhana , wanadharau sana yaani anafikiri wote ni wakijijini . we inawezekanaje uagize chakula wakati huna uhakuka na mfuko wako,  huu ni utapeli. Hapa haiwezekani yaani kwanz lazima tukufundishe adamu. Akamuita mhudumu  wake akamwambia piga simu polisi iliakaonje joto lajiwe.
Ndugu nikiwa najitetea moyoni nafsi yangu iliwaza sana huku nikijiuliza pesa ntakuwa nimeweka wapi, au nimedondoshea wapi na je itakuwaje nakoelekea maana ndo pesa niliyokuwa nayo pekee ambayo niliipigia hesabu kuwa nikifika siku ya kwanza ntalala chumba cha wageni kishantakula na baada ya usahiri nitawezarudi nyumbani kusubiria majibu. Hali ilikuwa tofauti na hapo abiria wote walishaingia kwenye Basin a mimi ndo pekee walikuwa wakinisubiri,
Nikiwa pale kaunta  nilisikia sauti ikisema kijana hebu njoo, kugeuka alikuwa ni yule jirani yangu wa Meza ambapo nilipokuwa  nimekaa nakula wao na familia yao walikuwa wamekaa jirani yangu. Nikaenda .akaniuliza kijana kulikoni. Kiukweli nilijikuta namuelezea kinaga ubaga bila kupepesa hata jicho na bila kuficha hata chembe ya neno au herufi moja kinywani mwangu.  Alinijibu sasa utafanyaje na pesa zote ushapoteza..! nikasema wala sijui  cha kufanya mpaka sasa.
Basi alinipatia kiasi cha pesa ambacho niliweza kulipa na  matumizi yote ya  Safari yangu huko nilipo kuwa na kwenda. Nilimshukuru na nikapanda ndani ya Basi japo abilia walikuwa wakinong’ona. Na wengine wakiwa wamekasirika . nilijisikia vibaya sana  maana kwanza mimi ndiye pekee waliyekuwa wananisubiri. Safari iliendelea.
Tukiwa njiani katikati ya Msitu mkubwa ambao ni hifadhi ndogo ya wanyama mara ghafla nilisikia sauti za abiria na konda wakishangaa. “Ayaa  mamaaaa….! “ Abiria wote tulihamaki kwa mshtuko na kutaka kujua kilichokuwa kinaendelea. Ilikuwa ni ajari ya gari dogo. Tulishuka na lilikuwa linateketea kwa moto chaajabu ndani ya Gari lile aliyenusurika ni mtoto mmoja ,ambaye nilipo mwangalia niligundua ni yule aliyekuwa na wazazi wake. Ni kasema maskini sasa wazazi wake wamekufa na  nina deni lakurejesha pesa ambayo niliazimwa  na kutakiwa kurudisha ofisini baada ya kurudi. Ofisi ambayo nilielekezwa  kwa kuandikiwa kwenye kikaratasi . sasa Deni hili nitamlipa nani?
 Na je huyu mtoto atalelewa na nani nIlimuomba Mungu kimoyomoyo amsaidie na kumtumnza mtoto yule. Lakini swali langu la msingi ni juu ya lile deni kuwa nitamlipa nani  wakati mwenye nayo ameteketea kwa moto nisijue hata ndugu zake. Na huyu mtoto amebaki peke yake nani atamlea na kumtunza akue. Maana mimi mwenyewe nimesaidiwa tu.
Safari iliendelea wasamalia wema walimchukua yule mtoto, nilienda nikamaliza intaview yangu  na kurudi . Siku zilipita  na niliyasahau yote  ukizingatia na interview yenyewe sikufanikiwa kupata kazi. Hivyonilijichanga mtaani na kidogo kidogo nilikusanya kiasi cha pesa nikafanikiwa kufungua ofisi yangu na kuajiri watu. kiujumla nilitengeneza walau kajina mtaani ambapo asilimia kubwa kaofisi kangu kalijulikana
Siku moja alikuja  kijana mmoja mwenye  umri yapata kama miaka 18 hivi alifika ofisini kwangu na kukutana na mtu wa mapokezi ambapo alijitambulisha na kueleza shida yake kuwa anataka kuonana na boss wa kampuni hii.
Basi  yule mfanyakazi wa mapokezi alikuja na kuniambia kuwa kunamtu  alikua na shida na mimi. Naomba nikuambie jambo hapa . kipindi hicho kilikua  ni kipindi ambacho ilikuwa ni vigumu sana kuniona kutokana na jeuri ya pesa niliyo kuwa nayo na jeuri ya lilejina la ama cheo cha Kuitwa Boss.  Sasa sijui ni nini kilinikuta siku ile , nikamwambia amruhusu aingie. Kijana aliingia na kunisalimia kwa upole sana  nikamkaribisha kwa ishara tu karibu kabla hajakaa nikawa nimeongea sentensi za kutosha ambazo zilionesha kumhuzunisha sana . nilimwambia sina muda wa kupoteza nina haraka hivyo ongea kwa kifupi shida yako na nikusikilize  maana nina appointment nyingi hivyo sina muda wa kupoteza.
Kijana alijikakamua  na kuniambia samahani naomba msaada wa pesa nikamtibu shangazi yangu ni mgonjwa hoi taabani.
Kiukweli alinikera sana nilimwangalia kwa hasira na nikajiuliza yaani huyu kijana ni mshenzi sana anawezaje kuvuka ofisi zote hizo na kushindwa omba msaada  yaani anafikiri hapa ni msikiti wa ijumaa ee..!.  “ hivi wewe kijana umetumwa au  yaaani ofisi zote umevuka umeona uje hapa kuomba msaada unadhani hapa ni msikiti wa ijumaa? Alinidakiza akasema Samahani  ila nimelazimika  kufanya hivi maana shangazi yangu ni mgonjwa na hakuna  ndugu yeyote wa kumsaidia. Kwani mimi wazaziwangu walisha famili mda.
 Nikajua huyu niyatima tu ambaye itakuwa wazazi wake waliangamia kwa maradhi ya kisasa yaaani UKIMWI,  nika muuliza wazazi wako walifariki lini. Akanijibu Tangu miaka kumi na mitano iliyopita  ambapo walikufa kwa ajari baada ya Gari tulilokuwa tumepanda kupata ajari na kuteketea kwa moto na mimi pekee kuponea chupu chupu. Tukiwa tunatoka Tabora Kuelekea Katavi.
Kusikia hivyo moyo ulilipuka nikajikuta nimeinuka kwa kasi kubwa kutoka kwenye kiti nilichokuwa nimekaa. Hali ambayo  hata kijana ilimshtusha na kumfanya aogope sana .”eti… nini” Baba yako aliitwa nani?” nilimuuliza.
Aliitwa Masala kulangwa. Alisema kijana ambaye alijitambulisha kwa jina la  alen masala kulangwa. Niliondoka kwa hatua ndefu kuelekea kwenye kabati ya majalada ya kumbukumbu na kutoa kijitabu kidogo ambacho nilikifungua , Mungu wangu  Hakika wakati wa kulipa deni umefika nilijisemesha moyoni. Aliniambia nikifika Tabora  nikiuliza  Masala Kulangwa nitaelekezwa hadi Ofisini kwake.
Nili muomba Mungu  kwa uchungu mkubwa sana, machungu yalinijaa moyoni.” Hakika tenda wema uende zako   na wakati wa Mungu ni wakati sahihi,
 Inawezekanaje Huyu kijana aje kwangu moja kwa moja na ni nani aliye muelekeza kuja hapa na je mda wote huo alikua wapi kuja au kuna mtu amemuongoz ana swali lililopita kwenye kichwa changu ilikuwa ni kwanini Mungu uliwachukua wazazi wake wakati ulijua kabisa nina deni la kulipa . ila niliishia kusema Asante sana Mungu maana wakati wa kulipa wema umefikia naahidi  kukulea kijana .
Nilirudi   taratibu na kumkumbatia yule kijana huku machozi ya uchungu yakinitoika nika sema . aleni mimi ni baba yako mdogo. Nitahakikisha unapata elimu na unamsaidia shangazi yako mpaka apone.
Aleni alibaki anastaajabu huku machozi yakimbubujika na wala asijue kinachoendelea na kinachosikiksa kwenye masikio yake.
Niliongozana naye mpaka kwa shangazi yake  Na nilimsimulia shangazi yake yote ,juu ya mkasa  mzima wa ajari nampaka sasa hali ilivyo. Shangazi alifurahia san asana.
Shangazi alikua na kansa ambayo ilikua hatua za mwisho. Nilihakikisha anapatiwa matibabu na akaruhusiwa kurudi nyumbani baada ya auheni . Maisha yakaendelea na alen akaendelea na shule maana hakuwa na Ada hivyo nililipa kila kitu , na maisha ya furaha yakarejea tena katika familia ya alen na shangazi yake. Ingawa baadaye Shangazi yake alifariki Dunia.
Nilijifunza kuwa  hakika Wema hauzozi na sikuzote malipo ya wema huwa ni hapa hapa Duniani. Nilitamani sana wazazi wa alen ambao miaka mingi walifariki kwa kuteketea kwa moto  wangalikuwepo walau wautazame wema na fadhila ambazo nimeitendea familia yao kwa fadhila  walizokuwa pia wamenisitiri kwenye utupu wa matusi  siku ile ya safari .
Ingawa nilijipa moyo kuwa furaha ambayo niliitengeneza kwa  aleni furaha hiyo piwa iliwafikia huko waliko na wameendelea kuwa na furan a nikasema kufariki kwa shangazi ni kama salamu za furaha ambazo amewapelekea wazazi wake na alen.
Eee Mungu nifundishe kuutambua wema  na  nifundishe siku zote kuushi wema huo ambao umenifanya niutambue kwa majirani zangu ama kwa rafiki zangu ama kwa wanadamu wenzangu kwa ujumla.
Na imenukuliwa kwa kujifunza zaidi


Read More

Thursday, October 5, 2017

SEKONDARI YA RUNGWA NA MPANDA GIRLS MKOANI KATAVI YAPOKEA ZAWADI YA MAJIKO BANIFU (4),TOKA KWA MKUU WA MKOA WA KATAVI

12:28:00 PM 0
MKUU wa Mkoa wa Katavi Meja Jenerali Mstaafu Raphael Muhuga,amekabidhi majiko banifu manne yenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni nne kwa shule za sekondari Rungwa na Mpanda Girls.


Akikabidhi majiko hayo ambayo yametolewa na mradi wa Usimamizi endelevu wa misitu ya miombo Tanzania,Muhuga amesema majiko hayo yanalenga kupunguza uharibifu wa mazingira.
Kwa upande wake mratibu wa mradi wa usimamizi endelevu wa misitu ya miombo taifa NPC Bw.Yobu Kiungo amesema, katika Mkoa wa Katavi mradi huo unatekelezwa Wilayani Mlele ambapo shule hizo zimepata majiko kutokana na kuwa katika makao makuu ya mkoa.

Awali akisoma taarifa ya mkoa,kaimu katibu tawala Msaidizi Mkoani Katavi Mhandisi Awariywa Moses Nnko amesema kwa mwaka 2017 mradi huo umewezesha majiko 983 yenye thamani ya shilingi milioni sitini yamewezeshwa katika taasisi za serikali na kaya binafsi.
Aidha Nnko amesema kuwa mwaka 2015/2016 mradi uliwezesha mashine mbili za umeme na mashine tanzu kwa ajili ya kuzalisha mkaa mbadala huku mwaka 2016/2017 mradi uliwezesha mtambo wa gesi asilia katika shule ya Sekonadri Inyonga kwa ajili ya kupika na matumizi ya maabara.

Wakati huo huo kwa Mwaka 2016/2017 mradi umewezesha majiko banifu 595 ya kiwemo ya kaya 7,Shule ya Mingi mtakuja jiko 1 na Shule ya Sekondari Inyonga 2.
Kwa upande wake mkuu wa Shule ya Sekondari Rungwa Emmanuel Cassian Mwamwezi na Nyabisye Sabasi mkuu wa Sekondari ya wasichana Mpanda Girls wamesema majiko hayo yamesaidia kurahisisha upishi wa vyakula vya wanafunzi na kutunza mazingira kwa kupunguza matumizi ya kuni.

 Mradio huo ulio chini ya Mpango wa Shirika la Maendeleo la Kimataifa UNDP pia unatekelezwa mkoani Tabora.
Dada mkuu wa shule ya sekondari ya wasichana ya Mpanda Girls Delila Ebanda akizungumza kwa niaba ya wanafunzi wa shule hiyo,asema majiko hayo watayatunza vizuri ili yatumike kwa wanafunzi watakaokuwepo katika shule hiyo hata baada ya wanafunzi waliopo kuhitimu.
Mkuu wa Wilaya ya Mpanda Bi.Lilian Charles Matinga,Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Manispaa ya Mpanda Mwalimu Enelia Lutungulu,Afisa elimu wa Mkoani Katavi Ernest Hinju na wataalamu wengi wa elimu kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Katavi na Wilaya ya Mpanda walikuwepo huku Manispaa ikiahidi kutunza majiko hayo.

Shule ya sekondari ya Rungwa yenye jumla ya wanafunzi 838 kati yao wasichana wakiwa ni 386 na wavulana 432 ina walimu 40 huku kwa upande wa shule ya sekondari ya wasichana ya Mpanda Girls iliyoanzishwa Februari 25 mwaka 1986 kwa sasa ina jumla ya wanafunzi 981 na walimu 40 kati yao walimu wa kike wako 9 na wa kiume 31.

Shule ya sekondari Mpanda Girls yenye mchepuo wa Tahasusi za PCB , PCM, CBG, EKA,HGE, EGM, HKL, HGK, NA HKL inafundisha masomo ya sayansi,uchumi na sanaa ambapo mwaka 2011 serikali iliipandisha hadhi ya kuchukua wanafunzi wa kidato cha 5 na 6 ambapo kuanzia mwaka 2005 ilikuwa ikichukua wanafunzi wa kidato cha tano pekee na kufundisha tahasusi ya HGK.

Read More

Post Top Ad

Your Ad Spot