MFUMO WA 'OPRAS' KWA WATUMISHI NI NJIA YA WAZI YENYE KULETA MABORESHO KATIKA SEKTA ZA UMMA (MAHAKAMA) - MAISHA ONLINE BLOG

Hot

Post Top Ad

Your Ad Spot

Tuesday, July 7, 2015

MFUMO WA 'OPRAS' KWA WATUMISHI NI NJIA YA WAZI YENYE KULETA MABORESHO KATIKA SEKTA ZA UMMA (MAHAKAMA)



OPRAS  ni mfumo wa wazi wa mapitio ya tathmini ya utendaji kazi pia ni utaratibu wa kumpima mtumishi utendaji wake wa kazi kwa kipindi cha mwaka mmoja ambapo katika utekelezaji huu upimaji hufanyika kwa lengo la mwajili na mtumishi katika kupanga mipango ya utekelezaji na kusimamia na kutathmini utekelezaji na kufanya mabadiliko ya utekelezaji yenye kuboresha utendaji katika taasisi  yakiwa naazma ya kufikia malengo ya taasisi kwa ujumla





Kwa mantiki hiyo Watumishi wa mahakama  wametakiwa kuzidi kufanya kazi kwa weredi mkubwa kulingana na nafasi walizo nazo ili kuleta ufanisi wa utekelezaji wa kila siku wa shughuli za  kimahakama  katika idara, vitengo na watumishi wote kama yalivyo katika mpango kazi wa mwaka




 
Akizungumza na watumishi wa mahakama wakati wa ufunguzi wa  kikao cha mwisho cha kufanya tathmini ya utendaji wa kazi mh.Jaji mfawidhi mkoa wa rukwa bw. kakusulo sambo  amesema mkoa wa rukwa ni moja kati ya mikoa bora inayochukua nafasi ya juu  kiutendaji katika kutekeleza majukumu ya kila siku ya mahakama
Kakusulo ameongeza kwa kusema kuwa mifumo ya kimenejiment ya utendaji inalenga kujenga uelewa wa  pamoja wa mahitaji ya maendeleo ya watumishi
Edward paul mbala nimkufunzi katika kikao hichi na pia ni mtendaji katika mahakama mkoani rukwa amesema  mfumo huu wa wazi wa OPRAS  unalenga kuletahali ya mtumishi kujitambua na kutekeleza majukumu yake kulingana na nafasi aliyonayo
Kwa upande wake bw.Leonard magacha   ambaye ni mtendaji wa mahaakama na mkufunzi katika mafunzo haya amezitaja faida za mfumo huu wa OPRAS kuwa ni pamoja nakumsaidia mtumishi kufahamu mapungufu yake kiujuzi na nini afanye katika kuboresha utendaji wake katika kazi
Pia mfumo huu unampa nafasi mwajiri kujikita zaidi katika utekelezaji wa malengo ya taasisi na kumwezesha kufahamu mahitaji ya kimaendeleo ya mtumishi na mpango wa jinsi ya kutumia rasilimali watu









No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot