OPRAS ni mfumo wa
wazi wa mapitio ya tathmini ya utendaji kazi pia ni utaratibu wa kumpima
mtumishi utendaji wake wa kazi kwa kipindi cha mwaka mmoja ambapo katika
utekelezaji huu upimaji hufanyika kwa lengo la mwajili na mtumishi katika
kupanga mipango ya utekelezaji na kusimamia na kutathmini utekelezaji na
kufanya mabadiliko ya utekelezaji yenye kuboresha utendaji katika taasisi yakiwa naazma ya kufikia malengo ya taasisi
kwa ujumla
Kwa mantiki hiyo Watumishi wa mahakama
wametakiwa kuzidi kufanya kazi kwa weredi mkubwa kulingana na nafasi
walizo nazo ili kuleta ufanisi wa utekelezaji wa kila siku wa shughuli za kimahakama katika idara, vitengo na watumishi wote kama
yalivyo katika mpango kazi wa mwaka
Akizungumza na watumishi wa mahakama wakati wa ufunguzi wa kikao cha mwisho cha kufanya tathmini ya
utendaji wa kazi mh.Jaji mfawidhi mkoa wa rukwa bw. kakusulo sambo amesema mkoa wa rukwa ni moja kati ya mikoa
bora inayochukua nafasi ya juu
kiutendaji katika kutekeleza majukumu ya kila siku ya mahakama
Kakusulo ameongeza kwa kusema kuwa mifumo ya kimenejiment ya
utendaji inalenga kujenga uelewa wa pamoja
wa mahitaji ya maendeleo ya watumishi
Edward paul mbala nimkufunzi katika kikao hichi na pia ni
mtendaji katika mahakama mkoani rukwa amesema mfumo huu wa wazi wa OPRAS unalenga kuletahali ya mtumishi kujitambua na kutekeleza
majukumu yake kulingana na nafasi aliyonayo
Kwa upande wake bw.Leonard magacha ambaye
ni mtendaji wa mahaakama na mkufunzi katika mafunzo haya amezitaja faida za
mfumo huu wa OPRAS kuwa ni pamoja nakumsaidia mtumishi kufahamu mapungufu yake
kiujuzi na nini afanye katika kuboresha utendaji wake katika kazi
Pia mfumo huu unampa nafasi mwajiri kujikita zaidi katika
utekelezaji wa malengo ya taasisi na kumwezesha kufahamu mahitaji ya
kimaendeleo ya mtumishi na mpango wa jinsi ya kutumia rasilimali watu
No comments:
Post a Comment