SIMULIZI LA WEMA HAUOZI
Nakumbuka ilikuwa ya pata miaka mingi iliyopita ambapoa
nililazimika kufunga safari kuelekea mkoani katavi Mkoa ambao naweza sema
kwangu mimi ulikua ni mkoa wa ahadi.
Nililazimika kwenda mara baada ya kumaliza chuo cha
upapalazi na huko ndiko ambapo kulikuwa na nafasi ya ajira , hivyo miongoni mwa
watu wengi ambao waliomba nafasi ya kazi kwenye kituo kimoja cha upapalazi.
Nami nilikuwemo.
Katika safari yangu nakumbuka nilikua nimepanda Basi kampuni
ya AMC nilikua natoka Tabora kuelekea mkoani katavi. Sauti ya konda ilisikika
ikisema tutatumia dakika kumi tu
kunywa chai na kuchimba dawa.
Nilistuka kwani kausingingizi
kalikuwa kamenipitia japo miaka hiyo ilikuwa ni ngumu sana kupata usingizi kama
umepanda Basikwa barabara ya
TABORA via KATAVI. Maana njia
ilikuwa si njia mabonde si mabonde
na mashimo barabara nzima.
Kwaharaka haraka kuhofia muda niliagiza chakula na nikaka kwenye meza moja ambayo
ilikua na viti vitatu lakini havikuwa na mtu ni mimi tu ndo nilikuwa hapo ingawaje pembeni yangu kulikuwa na meza
ambayo siti zilipambwa na familia ya baba na mama na mtoto mmoja walioonekana
ni wenye furaha na walikuwa wakipata chakula pamoja na vinywaji.
Basi nikaendelea kunywa na mara nilipo maliza nikaenda
kaunta ya chakula ilinilipe naingiza mfuko mara sioni pesa , pesa ambayo
nakumbuka ilikuwa nikiasi kidogo tu ambacho nilikikusanya kwa chasho la kuuza
mchicha, tena nakumbuka kipindi ambacho niko nyumbani tulianzisha bustani ya
mbogamboga kukidhi haja ya mahitaji madogomadogo . wakati mimi nikitumia nguvu
kubwa kuikusanya pesa hiyo iliniweze pata nauri ya kunipeleka kwenye ahadi ya ngu mpaya. Yaani mkoani Katavi
kwenye Usahiri.
Heee kilicho tokea sikuamini baada ya kumwambia mhudumu kuwa
siioni pesa nilikuwa na pesa mfukoni ssa siioni, ndugu. Niliporomoshewa matusi
ambayo sijawahi hata yasikia tangu utoto wangu, huku Boss wa eneo hilo akisema
vijana wasiku hizi bhana , wanadharau sana yaani anafikiri wote ni wakijijini .
we inawezekanaje uagize chakula wakati huna uhakuka na mfuko wako, huu ni utapeli. Hapa haiwezekani yaani
kwanz lazima tukufundishe adamu. Akamuita mhudumu wake akamwambia piga simu polisi iliakaonje joto lajiwe.
Ndugu nikiwa najitetea moyoni nafsi yangu iliwaza sana huku
nikijiuliza pesa ntakuwa nimeweka wapi, au nimedondoshea wapi na je itakuwaje
nakoelekea maana ndo pesa niliyokuwa nayo pekee ambayo niliipigia hesabu kuwa
nikifika siku ya kwanza ntalala chumba cha wageni kishantakula na baada ya
usahiri nitawezarudi nyumbani kusubiria majibu. Hali ilikuwa tofauti na hapo
abiria wote walishaingia kwenye Basin a mimi ndo pekee walikuwa wakinisubiri,
Nikiwa pale kaunta nilisikia sauti ikisema kijana hebu
njoo, kugeuka alikuwa ni yule jirani yangu wa Meza ambapo nilipokuwa nimekaa nakula wao na familia yao
walikuwa wamekaa jirani yangu. Nikaenda .akaniuliza kijana kulikoni. Kiukweli
nilijikuta namuelezea kinaga ubaga bila kupepesa hata jicho na bila kuficha
hata chembe ya neno au herufi moja kinywani mwangu. Alinijibu sasa utafanyaje na pesa zote ushapoteza..!
nikasema wala sijui cha kufanya
mpaka sasa.
Basi alinipatia kiasi cha pesa ambacho niliweza kulipa
na matumizi yote ya Safari yangu huko nilipo kuwa na
kwenda. Nilimshukuru na nikapanda ndani ya Basi japo abilia walikuwa
wakinong’ona. Na wengine wakiwa wamekasirika . nilijisikia vibaya sana maana kwanza mimi ndiye pekee
waliyekuwa wananisubiri. Safari iliendelea.
Tukiwa njiani katikati ya Msitu mkubwa ambao ni hifadhi
ndogo ya wanyama mara ghafla nilisikia sauti za abiria na konda wakishangaa. “Ayaa mamaaaa….! “ Abiria wote tulihamaki kwa
mshtuko na kutaka kujua kilichokuwa kinaendelea. Ilikuwa ni ajari ya gari dogo.
Tulishuka na lilikuwa linateketea kwa moto chaajabu ndani ya Gari lile
aliyenusurika ni mtoto mmoja ,ambaye nilipo mwangalia niligundua ni yule aliyekuwa
na wazazi wake. Ni kasema maskini sasa wazazi wake wamekufa na nina deni lakurejesha pesa ambayo
niliazimwa na kutakiwa kurudisha
ofisini baada ya kurudi. Ofisi ambayo nilielekezwa kwa kuandikiwa kwenye kikaratasi . sasa Deni hili nitamlipa
nani?
Na je huyu
mtoto atalelewa na nani nIlimuomba Mungu kimoyomoyo amsaidie na kumtumnza mtoto
yule. Lakini swali langu la msingi ni juu ya lile deni kuwa nitamlipa nani wakati mwenye nayo ameteketea kwa moto
nisijue hata ndugu zake. Na huyu mtoto amebaki peke yake nani atamlea na
kumtunza akue. Maana mimi mwenyewe nimesaidiwa tu.
Safari iliendelea wasamalia wema walimchukua yule mtoto,
nilienda nikamaliza intaview yangu
na kurudi . Siku zilipita
na niliyasahau yote
ukizingatia na interview yenyewe sikufanikiwa kupata kazi.
Hivyonilijichanga mtaani na kidogo kidogo nilikusanya kiasi cha pesa
nikafanikiwa kufungua ofisi yangu na kuajiri watu. kiujumla nilitengeneza walau
kajina mtaani ambapo asilimia kubwa kaofisi kangu kalijulikana
Siku moja alikuja
kijana mmoja mwenye umri
yapata kama miaka 18 hivi alifika ofisini kwangu na kukutana na mtu wa mapokezi
ambapo alijitambulisha na kueleza shida yake kuwa anataka kuonana na boss wa
kampuni hii.
Basi yule
mfanyakazi wa mapokezi alikuja na kuniambia kuwa kunamtu alikua na shida na mimi. Naomba
nikuambie jambo hapa . kipindi hicho kilikua ni kipindi ambacho ilikuwa ni vigumu sana kuniona kutokana na
jeuri ya pesa niliyo kuwa nayo na jeuri ya lilejina la ama cheo cha Kuitwa
Boss. Sasa sijui ni nini
kilinikuta siku ile , nikamwambia amruhusu aingie. Kijana aliingia na
kunisalimia kwa upole sana
nikamkaribisha kwa ishara tu karibu kabla hajakaa nikawa nimeongea
sentensi za kutosha ambazo zilionesha kumhuzunisha sana . nilimwambia sina muda
wa kupoteza nina haraka hivyo ongea kwa kifupi shida yako na nikusikilize maana nina appointment nyingi hivyo
sina muda wa kupoteza.
Kijana alijikakamua
na kuniambia samahani naomba msaada wa pesa nikamtibu shangazi yangu ni
mgonjwa hoi taabani.
Kiukweli alinikera sana nilimwangalia kwa hasira na
nikajiuliza yaani huyu kijana ni mshenzi sana anawezaje kuvuka ofisi zote hizo
na kushindwa omba msaada yaani
anafikiri hapa ni msikiti wa ijumaa ee..!. “ hivi wewe kijana umetumwa au yaaani ofisi zote umevuka umeona uje hapa kuomba msaada unadhani
hapa ni msikiti wa ijumaa? Alinidakiza akasema Samahani ila nimelazimika kufanya hivi maana shangazi yangu ni
mgonjwa na hakuna ndugu yeyote wa
kumsaidia. Kwani mimi wazaziwangu walisha famili mda.
Nikajua huyu
niyatima tu ambaye itakuwa wazazi wake waliangamia kwa maradhi ya kisasa yaaani
UKIMWI, nika muuliza wazazi wako
walifariki lini. Akanijibu Tangu miaka kumi na mitano iliyopita ambapo walikufa kwa ajari baada ya Gari
tulilokuwa tumepanda kupata ajari na kuteketea kwa moto na mimi pekee kuponea
chupu chupu. Tukiwa tunatoka Tabora Kuelekea Katavi.
Kusikia hivyo moyo ulilipuka nikajikuta nimeinuka kwa kasi
kubwa kutoka kwenye kiti nilichokuwa nimekaa. Hali ambayo hata kijana ilimshtusha na kumfanya
aogope sana .”eti… nini” Baba yako aliitwa nani?” nilimuuliza.
Aliitwa Masala kulangwa. Alisema kijana ambaye alijitambulisha
kwa jina la alen masala kulangwa.
Niliondoka kwa hatua ndefu kuelekea kwenye kabati ya majalada ya kumbukumbu na
kutoa kijitabu kidogo ambacho nilikifungua , Mungu wangu Hakika wakati wa kulipa deni umefika
nilijisemesha moyoni. Aliniambia nikifika Tabora nikiuliza
Masala Kulangwa nitaelekezwa hadi Ofisini kwake.
Nili muomba Mungu
kwa uchungu mkubwa sana, machungu yalinijaa moyoni.” Hakika tenda wema
uende zako na wakati wa
Mungu ni wakati sahihi,
Inawezekanaje
Huyu kijana aje kwangu moja kwa moja na ni nani aliye muelekeza kuja hapa na je
mda wote huo alikua wapi kuja au kuna mtu amemuongoz ana swali lililopita
kwenye kichwa changu ilikuwa ni kwanini Mungu uliwachukua wazazi wake wakati
ulijua kabisa nina deni la kulipa . ila niliishia kusema Asante sana Mungu
maana wakati wa kulipa wema umefikia naahidi kukulea kijana .
Nilirudi
taratibu na kumkumbatia yule kijana huku machozi ya uchungu yakinitoika
nika sema . aleni mimi ni baba yako mdogo. Nitahakikisha unapata elimu na
unamsaidia shangazi yako mpaka apone.
Aleni alibaki anastaajabu huku machozi yakimbubujika na wala
asijue kinachoendelea na kinachosikiksa kwenye masikio yake.
Niliongozana naye mpaka kwa shangazi yake Na nilimsimulia shangazi yake yote ,juu
ya mkasa mzima wa ajari nampaka
sasa hali ilivyo. Shangazi alifurahia san asana.
Shangazi alikua na kansa ambayo ilikua hatua za mwisho.
Nilihakikisha anapatiwa matibabu na akaruhusiwa kurudi nyumbani baada ya auheni
. Maisha yakaendelea na alen akaendelea na shule maana hakuwa na Ada hivyo
nililipa kila kitu , na maisha ya furaha yakarejea tena katika familia ya alen
na shangazi yake. Ingawa baadaye Shangazi yake alifariki Dunia.
Nilijifunza kuwa
hakika Wema hauzozi na sikuzote malipo ya wema huwa ni hapa hapa
Duniani. Nilitamani sana wazazi wa alen ambao miaka mingi walifariki kwa
kuteketea kwa moto wangalikuwepo
walau wautazame wema na fadhila ambazo nimeitendea familia yao kwa fadhila walizokuwa pia wamenisitiri kwenye
utupu wa matusi siku ile ya safari
.
Ingawa nilijipa moyo kuwa furaha ambayo niliitengeneza
kwa aleni furaha hiyo piwa
iliwafikia huko waliko na wameendelea kuwa na furan a nikasema kufariki kwa
shangazi ni kama salamu za furaha ambazo amewapelekea wazazi wake na alen.
Eee Mungu nifundishe kuutambua
wema na nifundishe siku zote kuushi wema huo ambao umenifanya
niutambue kwa majirani zangu ama kwa rafiki zangu ama kwa wanadamu wenzangu kwa
ujumla.
Na imenukuliwa kwa kujifunza zaidi
No comments:
Post a Comment