Mhe. Rais Dkt. John Pombe
Magufuli anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika maadhimisho ya siku ya
kimataifa ya kuongeza uelewa kuhusu ualbino yatakayofanyika katika
viwanja vya mnazi mmoja jijini Dar es Salaam.
Akiongea na waandishi wa habari
leo jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa chama cha Watu Wenye Ualbino
Nchini (Tanzania Albinism Society) Nemes Temba ameeleza kuwa kupitia
maadhimisho hayo jamii itapata fursa ya kupewa elimu muhimu kuhusu
ualbino ili kuondoka na dhana potofu hususani ushirikina.
“Maadhimisho haya ambayo yataanza
Juni 11 hadi Juni 13, 2016 yatasindikizwa na mambo mbalimbali ikiwemo
huduma za afya hususani uchunguzi na matibabu ya saratani ya ngozi
pamoja na nasaha za viongozi na mabalozi, utambulisho wa Miss Albino
Tanzania na uzinduzi wa kamusi ya ulemavu,” alisema Temba.
Temba aliendelea kuainisha kwamba
siku hiyo itawapa fursa watoto wenye ualbino waishio kwenye vituo
mbalimbali nchini kutembelea mji wa Bagamoyo kujionea mambo mbalimbali
chini ya ufadhili wa shirika la UNICEF.
Aidha Mwenyekiti huyo amemshukuru
Mhe. Rais Dkt. John Pombe Magufuli kwa kuwapa vipaumbele watu wenye
ulemavu akiwemo Dkt. Abdallah Possi ambaye ni Naibu Waziri Ofisi ya
Waziri Mkuu, Bunge, Sera, Ajira, Kazi na Watu Wenye Ulemavu hii
inadhihirisha kuwa ulemavu si hoja bali utendaji kazi ndio kitu umuhimu
No comments:
Post a Comment