Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi mkoa wa katavi
abdalah mselem ameitaka halmashauri ya
nsimbo wilaya ya mpanda kulirudisha mara moja gari la wagonjwa katika kituo cha
Afya cha katumba lililotolewa kwa msaada wa shirika linaloshughulikia wakimbizi
duniani UNHCR
Abdalah
mselem ameyasema hayo katika sherehe za uzinduzi wa maadhimisho ya chama
cha mapinduzi kutimiza miaka Arobaini zilizofanyika katika makazi ya wakimbizi
katumba.
Amesema sababu zinazotolewa na viongozi wa
halmashauri ya nsimbo kuwa gari hilo linapaswa kuwa ofisi za mkurugenzi wa
halimashauri hiyo sio za msigi na zinakiuka makubaliano ya wadhamini.
![](file:///C:\Users\user\AppData\Local\Temp\msohtmlclip1\01\clip_image002.gif)
Aidha amewataka viongozi wa chama cha mapinduzi
kusimamia vema ilani ya chama kwa kuondoa kero na changa moto mbalimbali za
wananchi ikiwa ni pamoja na huduma muhimu za kijamii kama vile Afya Elimu na
Miundo mbinu ya barabara
Sherehe za kutimiza miaka Arobaini ya chama cha
mapinduzi zinatarajiwa kuadhimishwa tarehe tano mwezi wa pili mwaka huu na
kimkoa zitafanyika katika makazi ya wakimbizi mishamo.
No comments:
Post a Comment