Kijana mmoja 44, Mkazi wa Sakalilo kata ya ilemba,ameuawa kwa kukatwa na kitu chenye ncha kali kichwani kisogoni na kisha kutupwa chini ya daraja la mto Mumba na watu wasiojulikana.
marehemu huyo aliye julikana kwa jina la KALTUS JACOB,ni mfipa na ni mkazi wa kijiji cha sakalilo kata ya ilemba tarafa a kipeta wilaya ya laela mkoani Rukwa.
Aidha kabla ya
tukio marehemu alionekana akiwa kilabuni na wake zake wawili wakinywa pombe na
aliwaaga na kuondoka na hakurudi tena hadi alipokutwa akiwa amefariki.
Chanzo cha mauaji
hakijajulikana juhudi za Jeshi la Polisi zinaendelea ili kubaini kiini cha
mauaji hayo.
Mwili wa marehemu
umekabidhiwa kwa ndugu zake kwa ajili ya mazishi mara baada ya kufanyiwa
uchunguzi wa kidaktari na kugundua kuwa alichomwa na kitu chenye ncha kali na
kutupwa mtoni.
Watuhumiwa
hawajakamatwa na uchunguzi unaendelea ili kuweza kuwabaini waliohusika katika
mauaji hayo.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Rukwa
Kamishna Msaidizi wa Polisi GEORGE SIMBA
KYANDO ametoa wito kwa wananchi kuwa atalifuatilia suala hilo na atahakikisha
wamekamatwa na kufikishwa katika vyombo vya sheria kwa hatua zaidi.
Aidha anatoa
ushauri kwa wananchi waweze kushirikiana na Jeshi la Polisi kwa kutoa taarifa
katika vituo vya Polisi vilivyo karibu nao ili kuweza kurahisisha kazi ya
kupambana na wahalifu na kuzuia uhalifu.
No comments:
Post a Comment