Rais Jakaya Mrisho Kikwete amezindua meli mbili kubwa za kisasa za kivita zenye meta 60, mizinga mikubwa miwili na ya kawaida sita kila moja, na uwezo wa kupiga makombora umbali wa kilometa saba angani na kilometa tisa chini ambazo zitakazowezesha usalama wa uhakika katika ukanda wa bahari wa Tanzania dhidi ya maharamia.
Mara
baada ya uzinduzi Rais. Kikwete amezikabidhi kwa kamandi ya jeshi la
wanamaji hafla iliyofanyika makao makuu ya kamandi hiyo yaliyopo
kigamboni jijini Dar es salaam ambapo amesema meli hizo zinafanya
Tanzania iandike historia mpya ya kuwa na meli kubwa na za kisasa kwa
mara ya kwanza nchini.
Akizungumza
katika uzinduzi huo waziri wa ulinzi na jeshi la kujenga
taifa,Dk.Hussein Mwinyi, amesema, meli hizo zitakuwa tegemeo kubwa
katika kulinda eneo la maji ya tanzania na rasilimali zake ikiwamo gesi
asililia,samaki kwani zina uwezo wa kasi kubwa katika kukabiliana na
vitendo vya uhalifu hasa uharamia.
Mkuu
wa majeshi ya ulinzi na usama nchini, Jenerali Davis Mwamunyange,
amesema,lengo la kuwa na meli za jinsi hiyo ni katika jitihada za
kuhakikisha jeshi linakuwa na silaha za kisasa za kivita na kutoa
mafunzo huku balozi wa china nchini, Lui Youging, akimpongeza Rais
Kikwete kwa jitihada za kuimarisha ulinzi wa taifa lake.
Meli
hizo zimepewa majina ya melivita P77 Mwitongo kuwakilisha eneo
alilozaliwa kiongozi wa kwanza wa Tanzania, hayati Julius Nyerere na
melivita P78 Msoga, eneo alilozaliwa Rais Kikwete ambaye anatarajia
kumaliza kipindi chake cha uongozi Novemba mwaka huu.
No comments:
Post a Comment