MKUU WA MKOA RUKWA: TUMIENI WELEDI WENU ILI KUPATA VIONGOZI BORA WA BAADAYE - MAISHA ONLINE BLOG

Hot

Post Top Ad

Your Ad Spot

Tuesday, April 28, 2015

MKUU WA MKOA RUKWA: TUMIENI WELEDI WENU ILI KUPATA VIONGOZI BORA WA BAADAYE

Kufuatia kutangazwa kwa  nafasi ya ajira ya ualimu kutoka ofisi ya wazili mkuu TAMISEMI  hapa nchini , serikali mkoni hapa imewataka waalimu kutumia fulsa hiyo ya ajira kwa kufanya  kazi kwa jitihada wawapo katika vituo vyao walivyopangiwa 



Akizungumza na chanzo hiki mkuu wa mkoa wa rukwa injinia stella martini manyanya amesema  fulsa walizo pata  walimu  wanatakiwa kuzitumia kulingana na weledi wao walioupata wawapo vyuoni na badala yake kutozifanyia mzaa ili ziwe chachu na faida kwa wazawa mkoani hapa




Aidha ameongeza kwa kukemea  tabia ya watu kuja  na kuomba nafasi za ajira  mkoani hapa na baada ya muda mfupi  kuomba uhamisho wa kubadilishiwa kituo cha kazi mkoa mwingine kwani kwa kufanya hivyo ni kuzichezea fulsa na kunyima nafasi wengine ambao ni wahitaji wa fulsa hiyo

Venance kusongwa ni mkuu wa chuo cha ualimu mkoa wa  rukwa ambaye  amewataka waalimu  kuyaishi maadili mema katika jamii ili waweze kuwaanda wanafunzi kuwa viongozi bora wanchi ya Tanzania na kwingineko duniani

 


 Lakini suala likabaki  kwa wanafunzi ambao bado wako vyuoni  katika chuo hicho cha ualimu rukwa wao wanazungumziaje ajira hii ya ualimu na nini matazamio yao baada ya kuhitimu















OFISI YA WAZIRI MKUU TAMISEMI INATANGAZA ORODHA
YA WANACHUO WAHITIMU WA MAFUNZO YA UALIMU KAMA
IFUATAVYO:-
i. Walimuwa Cheti (Daraja IIIA) kwa ajili ya shule za msingi 17,928
ii. Walimu wa Stashahada kwa ajili ya shule za sekondari 5,416
iii. Walimu wa Shahada kwa ajili ya shule za sekondari 12,677

Walimu hawa wamepangwa katika Halmashauri na shule za mazoezi za
vyuo vyaualimu Tanzania Bara.
 

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot