SASA NI MWENDO WA DIJITALI KWA MKOA WA RUKWA MJINI SUMBAWANGA - MAISHA ONLINE BLOG

Hot

Post Top Ad

Your Ad Spot

Saturday, March 28, 2015

SASA NI MWENDO WA DIJITALI KWA MKOA WA RUKWA MJINI SUMBAWANGA



MAMLAKA YA MAWASILIANO TANZANIA IMEWAAGIZA WATOA HUDUMA ZA USAMBAZA  WA VING`AMUZI MKOANI RUKWA  KUHAKIKISHA  KUWA KUNAKUWA NA VING`AMUZI VYA KUTOSHA ILI KUWAWEZESHA WANANCHI KUENDELEA KUPATA HUDUMA YA MATANGAZO MARA TU ZOEZI LA UZIMAJI WA MITAMBO YA KURUSHA MATANGAZO YA TELEVISHENI YA MFUMO WA ANALOJIA  LITAKAPO FANYIKA MAPEMA MARCH 31 MWAKA HUU


AKIZUNGUMZA NA VYOMBO VYA HABARI MKOANI HAPA ENJINIA LILIAN MWANGOKA  AMBAYE NI MENEJA NYANDA ZA JUU KUSINI AMESEMA WANANCHI HAWANA BUDI KUKABILIANA NA MABADILIKO YA  MFUMO KUTOKA ANALOJIA KWENDA DIJITALI ILI KUFULAHIA HUDUMA  YA MATANGAZO YANAYORUSHWA KWA MFUMO WADIJITALI

AIDHA AMEONGEZA KWA KUWATAKA WANACHI MKOANI HAPA  KUTOTUPA TV ZAO ZA ANALOJIA BADALA YAKE KUNUNUA VING`AMUZI ILI KUPATA MATANGAZO YA DIJITALI KWANI MABADILIKO HAYA HAYAHUSU MATANGAZO KWA NJIA YA SATELAITI, WAYA(CABLE)  NA REDIO
AIDHA AMEONGEZEA KWA KUSEMA KUWA MAANDALIZI YA UZIMAJI WA MATANGAZO KWA NJIA YA ANALOJIA UMEKAMILIKA KWA MJI WA SUMBAWANGA KWA KUWASHIRIKISHA WADAU WA SEKTA YA  UTANGAZAJI MAMBAPO  MITAMBO INATARAJIWA KUZIMWA SAA SITA USIKU WA TAREHE 31 MWEZI WA TATU MWAKA HUU ILI KURUHUSU MATANGAZO KWA NJIA YA DIJITALE KUANZA MKONI HAPA
 UZIMAJI WA MITAMBO KWA NJIA YA ANALOJIA  KWA AWAMU YA KWANZA ULIANZA KUTEKELEZWA NCHINI TAREHE 31.12.2014 KATIKA JIJI LA DAR ES SALAAMU KWA MAKUBALIANO YA NCHI WANACHAMA  WA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot