“Kwa
jina naitwa Israeli, lakini si yule mtoa roho za watu, hili ni jina
ambalo linapatikana katika utaratibu wa maisha ya kila siku duniani.
Nimezaliwa mwaka 1950, (kwa sasa 2010 ana miaka
60) wilayani Misungwi, mkoani Mwanza, ni mtoto wa kwanza katika familia
yenye kujiweza kidogo kimaisha, ikiwa na watoto tisa, wote wanaume.
Wazazi wangu (sasa marehemu) walikuwa wacha Mungu sana.
Kama kweli kuna uhai baada ya kifo na wakayajua mambo yangu ya duniani, naamini nimewaumiza sana wazazi wangu.
Kwa sasa naishi Mbagala, jijini Dar es Salaam na
familia yangu yenye mke na watoto saba, wote wa kike. Mke wangu pia kwao
ni mtoto wa kwanza katika familia yenye watoto tisa, wote wanawake.
Nimelazimika kusimulia mkasa huu wa kichawi baada
ya watu wengi kusimulia mikasa yao wakidai waliwahi kuwa wachawi
wakaacha kwa sababu mbalimbali ambazo wengine huzisema, wengine hufanya
siri kubwa.
Naweza kusema kwamba, karibu wote waliokuwa
wakisimulia maisha yao ya kichawi na mikasa yake, hakuna hata mmoja
aliyewahi kufikia hata robo ya maisha ya kichawi ya kwangu.
Mimi niliishi maisha hayo kwa miaka kumi, na
nilifika ‘levo’ ya mbali, mfano kuwa Mkuu wa Kikundi na kusafiri sehemu
mbalimbali duniani kwa ajili ya mikutano mikubwa ya kimataifa ya
wachawi.
Niliporudi, nilikuwa nakutana na wachawi wakubwa wa hapa nyumbani
Tanzania na kuwapa maagizo ya utendaji katika makundi yao sehemu
mbalimbali za nchi.
Katika kipindi chote cha kuwa mchawi nilibaini
mambo makubwa mawili, kwamba, maisha ya wachawi katika ulimwengu wao
hayana tofauti yoyote na maisha ya watu wasio wachawi katika ulimwengu
huu wa macho ya kawaida.
Maandiko yanaposema kuwa, Mungu aliumba vitu
vinavyoonekana na visivyoonekana ni kweli kabisa. Wachawi wanaamini
kwamba, vitu visivyoonekana pia vilikuwa na siku sita katika uumbaji wa
Mungu, siku ya saba akapumzika.
Na hiyo ndiyo sera ya mchawi mara tu baada ya kujiunga katika kazi hiyo inayolaaniwa na wengi ulimwenguni kote.
Kabla sijaenda mbele zaidi nataka kusema kuwa,
kama kuna shughuli mbalimbali za binadamu zinazoonekana kwa macho ya
kawaida duniani, pia kuna shughuli kama hizo hizo zisizoonekana kwa
macho ya kawaida, lakini zinashirikisha wachawi na mambo yao.
Itaendelea Mukinipa
Post Top Ad
Your Ad Spot
Monday, November 23, 2015
Home
Unlabelled
SIMULIZI LA KUSISIMUA'NCHI YA WACHAWI'
SIMULIZI LA KUSISIMUA'NCHI YA WACHAWI'
About JN POWER TV
Templatesyard is a blogger resources site is a provider of high quality blogger template with premium looking layout and robust design. The main mission of templatesyard is to provide the best quality blogger templates which are professionally designed and perfectlly seo optimized to deliver best result for your blog.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post Top Ad
Your Ad Spot
No comments:
Post a Comment