JAMII INAMCHANGO GANI KATIKA KUSAIDIA WAJANE NCHINI? - MAISHA ONLINE BLOG

Hot

Post Top Ad

Your Ad Spot

Tuesday, June 23, 2015

JAMII INAMCHANGO GANI KATIKA KUSAIDIA WAJANE NCHINI?


SIKU ya Wajane Duniani imeadhimishwa kwa mara ya kwanza tangu kuanzishwa kwake leo katika Viwanja vya Mashujaa, Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.
Katika sherehe hiyo mgeni rasmi alikuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Jinsia Wanawake na Watoto, Anna Maembe  aliyemwakilisha Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba, Maendeleo na Makazi, Angela Kairuki.
Akihutubia wakati wa maadhimisho hayo yaliyohudhuriwa na wajene wengi, mama Maembe alisema kuwa, maadhimisho hayo ya yalianza kuadhimishwa Juni 23, 2010 na hapa nchini yalianza rasmi kuwa na wanachama Juni 23 mwaka jana.
Aliongeza  kuwa Chama cha Wajane kimeanza kuadhimisha siku hiyo lengo likiwa ni kuwasaidia katika kutatua matatizo yao na kuwa nao karibu, hivyo na kuhakikisha wanasimamia haki zao kikamilifu ili kuepuka migogoro baada ya kuondokewa na waume zao.
Na :aloyce sengasenga
TOA MAONI YAKO HAPA

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot