halafu wanasema leo ni siku ya vyoo duniani ambapo mataifa ulimwenguni likiwemo la tanzania eti tunaadhimisha siku ya vyoo duniani
jamani aina hiyo ya choo kweli bado tunaendelea kuadhimisha siku hii kweli?
Leo ni siku ya choo duniani inayoratibiwa na Umoja wa Mataifa huku kukitolewa wito wa kuboresha mazingira na kuzingatia usafi wa vyoo vyenyewe. George Njogopa na taarifa zaidi
Siku hii ya choo duniani inakumbusha ulimwengu kuwa watu zaidi ya bilioni 2.5 duniani kote wanakabiliwa na matatizo yanayoambatana na ukosefu wa vyoo vinavyokithi mahitaji ya wakati hatua ambayo inawaweka kwenye mazingira ya kukumbwa na matatizo ya kiafya.
Ripoti moja iliyotolewa na Umoja wa Mataifa kuambatana na
siku hii inawataja wanawake na wasichana kuwa ndiyo walioko kwenye kundi
hatarishi la kukubwa na matatizo ya kiafya na inataka kuwekwa msukumo
wa kubadili hali hiyo
Ripoti hiyo imebainisha kuwa kila kwenye wanawake watata, basi mmoja
amekumbwa na matukio ya kama vile yanayodharirisha utu wake,kunyanyasika
hata kushambuliwa kutokana na kukosa sehemu salama ya kupata choo.Inasadikika kuwa, zaidi ya wanake milioni 526 duniani kote wanakosa faragha ya kwenda kijisaidia hatua inayowalazimu kwenda maeneo ya wazi kwa ajili ya kupata choo.
shime tuchukue hatua za lazima kuhakikisha kila mtanzania anaishi katika mazingira huku suala la choo akilipa kipaumbele cha kwanza
No comments:
Post a Comment