ni kweli wewe ni ndugu yangu lakini kwanini kila kitu wewe

lakini nafsi inaniuma sana nionapo unavyobadilika kama kinyonga asiye na aina moja ya rangi. sawa wahenga huwa ni kawaida yao na misemo yao kiukweli huwa hawachoki kusema ' KWELI KUWA UYAONE"
Ndiyo unapoa anza kuota ndevu haijarishi ni sehemu gani akili nayo hubambaruka na kusahau upendo wangu, chozi langu lililokuwa likimwagika kwaajiri yako
sawa lakini bado narudia kuwa wewe ni ndugu yangu
Tazama juzijuzi tu ulimwengu umekuonesha njia ukaamini kabisa yote uliyo yapata ni kwanguvu zako, lakini kwanini hukukumbuka kipindi ulipo lia na kuomba msaada kwangu? au ulikuwa una igiza sanaa za mapokeo tu.... ni kweli unajivika ngozi ya kondoo wakati u mbwamwitu wa mwitu.
Jamani kila tunalolifanya tuwe tunajaribu kukumbuka nguzo msingi za kimaisha maana bila baba,mama, kaka, dada,na ndugu ni hakika tusingali kuwa hapa;
wewe ni ndugu yangu na utabaki kuwa ndugu yangu
No comments:
Post a Comment