KUPATWA KWA JUA NI NINI? JIFUNZE HAPA - MAISHA ONLINE BLOG

Hot

Post Top Ad

Your Ad Spot

Wednesday, August 31, 2016

KUPATWA KWA JUA NI NINI? JIFUNZE HAPA

Kupatwa kwa jua kunatokea kama dunia, mwezi na jua vyote kwa pamoja vitakaa kwenye mstari mmoja mnyoofu yaani wakati mwezi unapita kati ya dunia na jua.

Katika hali hiyo kuna kivuli cha mwezi kwenye uso wa dunia. Kivuli hiki hakifuniki dunia yote. Kwa hiyo kupatwa kwa jua kunaonekana kwa watu wengi kama kupungua kwa mwanga wa jua.
Kisayansi kuna aina mbalimbali za kupatwa kwa jua. Miongoni mwa aina hizo ni kupatwa kwa jua kabisa;  hii jua ninapotea kabisa kwa dakika chache. Hali hii huonekana kwenye kanda nyembamba duniani kinapopita kitovu cha kivuli.
Aina nyingine ya kupatwa kwa jua ni kupatwa kipete; hapa mwezi huonekana mdogo kuliko jua. Hivyo duara la kung'aa kwa jua huonekana kubwa kuliko duara la mwezi na mwanga wa jua waonekana kama pete.
Pia aina nyingine ni kupatwa kwa jua kisehemu; hapa ni kuwa eneo kubwa la kivuli cha kando watu huona upungufu wa mwanga. Kiasi chake hutegemea umbali na kitovu cha kivuli. Ukitazama jua kwa filta kwa mfano kioo kilichopakwa dohani katika moshi wa mshumaa huwa wanaona sehemu ya duara ya jua imefunikwa.

Miongoni mwa aina hizo tatu za kupatwa kwa jua, huenda msomaji ulisha wahi kuona aina hizi kutegemea na umri wako. Laiki kwa kizazi cha sasa sina hakika sana kama wamewahi kuona aina hizo za kuaptwa na jua.
Mwezi Septemba mwaka huu kunatarajiwa kutokea tukiko kubwa la angani la kipekee la kupatwa kwa jua usawa wa Tanzania ambalo litatokea Septemba 1, mwaka huu, kuanzia saa 4:17 asubuhi hadi Saa 7:56 adhuhuri.
Washabiki na wanataaluma wa anga kutoka duniani kote pamoja na wanasansi, wanafunzi pamoja na jamii ya watanzania wanaelekea Wilayani Mbarali katika Kata ya Rujewa, mkoani Mbeya kushuhudia duara la jua linavyobadilika kuwa pete ya jua.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot