ABDALLA MSELEM KATAVI:GARI LA WAGONJWA LIRUDISHWE MARA MOJA : - MAISHA ONLINE BLOG

Hot

Post Top Ad

Your Ad Spot

Monday, January 30, 2017

ABDALLA MSELEM KATAVI:GARI LA WAGONJWA LIRUDISHWE MARA MOJA :



Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi mkoa wa katavi abdalah mselem  ameitaka halmashauri ya nsimbo wilaya ya mpanda kulirudisha mara moja gari la wagonjwa katika kituo cha Afya cha katumba lililotolewa kwa msaada wa shirika linaloshughulikia wakimbizi duniani UNHCR

Abdalah  mselem ameyasema hayo katika sherehe za uzinduzi wa maadhimisho ya chama cha mapinduzi kutimiza miaka Arobaini zilizofanyika katika makazi ya wakimbizi katumba.
Amesema sababu zinazotolewa na viongozi wa halmashauri ya nsimbo kuwa gari hilo linapaswa kuwa ofisi za mkurugenzi wa halimashauri hiyo sio za msigi na zinakiuka makubaliano ya wadhamini.
Aidha amewataka viongozi wa chama cha mapinduzi kusimamia vema ilani ya chama kwa kuondoa kero na changa moto mbalimbali za wananchi ikiwa ni pamoja na huduma muhimu za kijamii kama vile Afya Elimu na Miundo mbinu ya barabara
Sherehe za kutimiza miaka Arobaini ya chama cha mapinduzi zinatarajiwa kuadhimishwa tarehe tano mwezi wa pili mwaka huu na kimkoa zitafanyika katika makazi ya wakimbizi mishamo.  

    

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot