Mkuu wa
wilaya ya nkasi mh. Iddi kimanta Amewataka wanachama wa VICOBA (village community bank) kuzidi kujiimarisha katika vikundi vyao ili kufukia malengo kusudiwa
Akizungumza kwaniba
ya mkuu wa mkoa kwenye semina ya mpango
wa vicoba kwa maafisa wa mkoa wa rukwa ulio jumuisha maafisa wa halmashauri
zote za sumbawanga mh kimanta amesema
vikundi hivi vinaumuhimu mkubwa katika jamii kwani lengo kubwa la
kuanzishwa kwake ni kusaidia wanajamii kiuchumi na katika shughuli mbalimbali
za jamii
Kimanta
ameviasa vikundi hivi kutotoafulsa kwa wanasiasa kuvitumia kama jukwaa la kunadi sera zao hasa
katika kipindi hiki cha kampain tunapoelekea uchaguzi mkuu
Aidha kwa
upande wake bw. aldo mfinde ambaye ni mratibumtendaji wa asasi ya UYACODE – Taifa amezifafanua
faida za kujiunga na vikoba kuwa
ni pamoja na kujiwekea akiba kubwa itakayo wawezesha kupata mikopo mikubwa,
Faida
nyingine ni mwana kikundi kujijengea tabia ya kuweka akiba kila wiki ambayo itampa tija kubwa kwa maendeleo yake
na jamii
Banki hii ya
kijamii vijijini ni mpango unaotumia mfumo wa MMD (MATA MASU DUBALA) ulioanzishwa na shirika la Care
internetiona nchini niger 1991 unatoa fulsa ya mwanajamii kumiliki mtaji na
riba tofauti na mifumo mingine ya ukopeshaji fedha ambapo umiliki ni wa mkopeshaji
na mkopaji anakuwa kama chombo cha
kumzalishia faida mkopeshaji
TAZAMA PICHA ZA WAHIRIKI HAPA CHINI
No comments:
Post a Comment