ACT Walia kiongozi wao kuuawa......KIONGOZI ALIYE CHINJWA KINYAMA NA VIUNGO VYAKE KUPIKWA KWENYE SUFURIA - MAISHA ONLINE BLOG

Hot

Post Top Ad

Your Ad Spot

Monday, January 26, 2015

ACT Walia kiongozi wao kuuawa......KIONGOZI ALIYE CHINJWA KINYAMA NA VIUNGO VYAKE KUPIKWA KWENYE SUFURIA




CHAMA cha ACT-Tanzania kimelitaka Jeshi la Polisi nchini kuwasaka na kuwafikisha kwenye vyombo vya sheria wote waliohusika na tukio la mauaji ya aliyekuwa Mwenyekiti wa Kitongoji cha Masigo wilayani Mlele mkoani Katavi, Christian Kahongo. 

 

Taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa jana na Katibu Mkuu wa ACT-Tanzania, Samson Mwigamba, ilieleza kuwa chama hicho kinalaani mauaji hayo ya kinyama ambayo hayaendani na haki za binadamu.
 
Alisema walimkata kichwa na kukitenganisha kabisa na kiwiliwili kisha wakakata sehemu za siri na baadhi ya viungo vingine vya kichwa wakaanza kuvikaanga kwenye sufuria.
 
Alisema huo ulikuwa ni unyama wa ajabu ambao hatujawahi kuushuhudia.
Tukio hilo la mauaji ya kinyama lilitokea Januari 24, mwaka huu ambapo watu wasiojulikana walivamia nyumbani kwa Christian Kahongo na kumuua kwa kumkatakata mapanga.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot