WANAFUNZI ST. MAURUS WAASWA KUJIKITA KATIKA SALA NAKUSOMA KWA BIDII MKONI RUKWA - MAISHA ONLINE BLOG

Hot

Post Top Ad

Your Ad Spot

Monday, January 26, 2015

WANAFUNZI ST. MAURUS WAASWA KUJIKITA KATIKA SALA NAKUSOMA KWA BIDII MKONI RUKWA


 
 
 
 

 



 

 

 


WANAFUNZI  MKOANI RUKWA WAMETAKIWA KUJIBIDIISHA KATIKA ELIMU NA KUMTEGEMEA MWENYEZI MUNGU KWA SALA NA MAOMBI KATIKA MASOMO YAO NA BADALA YAKE KUEPUKANA NA VITENDO VIOVU  VITAKAVYO WAPELEKEA KUHARIBU MASOMO YAO NA BADALA YAKE KUSHINDWA KUFANYA VIZURI KATIKA MASOMO YAO
 
 
 
 
KAURI HIYO IMETOLEWA NA MH. BABA ABATE WA ABASIA YA ROHO MT. MVIMWA  DENIS NDOMBA WAKATI ALIPO ONGOZA IBADA YA MISA KWAAJIRI YA KUMBUKUMBU YA  MT.MAURUS  AMBAYO HUADHIMISHWA KILA MWAKA TAREHE26.01 ILIYOFANYIKA KATIKA SEKONDARI YA MT.MAURUS   AMBAPO AMEWASIHIWANAFUZI  KUIGA MAISHA YA SOMO WAO KATIKA KUFANYAKAZI, KUSOMA NAKUSALI ILI KULETA AMANI NA MAENDELEO NCHINI NA  TAIFA KWA UJUMLA





BABA ABATE  AMEONGEZA KWA KUONESHA KUWA WATAWA WANAKUMBANA NACHANGAMOTO MBALIMBALI KATIKA MASHIRIKA MBALIMBALI  NA AMEYAOMBA MASHIRIKA HAYO KUREJEA NYUMA NA KUFATA HISTORIA ZA WAANZILISHI KWA MAMBO WALIYOKUWA WANAPENDELEA NA KUIGA  MIFANO YAO ILI KUWA KAMA FAMILIA MOJA KATIKA USHIRIKIANO NA UELEWANO ILI KULIENDELEZA KANISA KATOLIKI KIIMANI NA UPENDO



AIDHA KWA UPANDE WAKE MKUU WA SHULE YA MT. MAURUS   BW.SIMONI KOMBA AMEELEZEA MIKAKATI MBALIMBALI INAYOFANYWA NA SHULE HIYO KATIKA KUHAKIKISHA KUWA MWAKA HUU WA MASOMO 2015 WANAFUNZI WANAFANYA VIZURI  KATIKA MASOMO YAO KWA KUONGEZA  VITABU VYA MASOMO YA HESABU KWA KILA MWANAFUNZI  NA KUONGEZA VIPINDI VYA ZIADA NYAKATI ZA JIONI ILI WANAFUNZI  WASIO NAUWEZO MZURI DARASANI WAPATE NAFASI YA KUELEWA ZAIDI




 
 







 


No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot