Serikali imezipiga marufuku shule binafsi nchini kuwafukuza ama kuwasitishia masomo wanafunzi wanaoshindwa kufikia wastani na kwamba shule zote zitakazokiuka agizo hilo zitachukuliwa hatua kali ikiwa ni pamoja na kufutiwa usajili.
Serikali pia imesema kuwa kuanzia mwaka 2016 itaanza kutoa elimu bure kuanzia shule ya msingi hadi kidato cha Nne.
Onyo hilo la serikali kwa wamiliki wa shule binafsi za serikali limetolewa na waziri wa elimu na mafunzo ya ufundi bungeni mjini Dodoma katika kikao cha kwanza cha mkutano wa 18 ulianza Dodoma katika kipindi cha maswali na majibu kutokana na swali la msingi la Mh Conchesta Rwamlaza.
Waziri huyo amesema ni marufuku kwa mameneja na wamiliki wa shule binafsi za sekondari kukaririsha, kuhamisha ama kuwafukuza shule wanafunzi wanaoshindwa kufikia wastani wa shule husika kwa kuwa kiwango cha ufaulu kilichowekwa na serikali ni wastani wa asilimia 30.
Aidha mbunge wa handeni Dr Henry Shekifu ameitaka serikali kutoa tamko la lini itaanza kutoa elimu bure ya kuanzia elimu ya msingi hadi kidato cha nne ili kuwawezesha watoto wote wa Tanzania kupata elimu ambapo serikali imesema utekelezaji wake utaanza mwakani.

No comments:
Post a Comment