MVUA KUBWA YAHALIBU MALI NA KUWAACHA WANANCHI BAADHI WA KATA YA SENGA MKOANI RUKWA BILA MAKAZI YA KUISHI - MAISHA ONLINE BLOG

Hot

Post Top Ad

Your Ad Spot

Wednesday, November 18, 2015

MVUA KUBWA YAHALIBU MALI NA KUWAACHA WANANCHI BAADHI WA KATA YA SENGA MKOANI RUKWA BILA MAKAZI YA KUISHI

 Mvua kubwa zinazoendelea kunyesha hapa nchini, zimepelekea kufanya uharibifu mkubwa wa mali na nyumba za wakazi waishio kata ya Senga wilaya ya sumbawanga mjini mkoa wa rukwa na kuwaacha baadhi ya wakazi kukosa makazi ya kuishi
katika adha hiyo nyumba pamoja na mali za ndani sambamba na mtoto  mdogo aliye kuwa amelala ndani kuangukiwa na sahemu ya kuta ya nyumba hiyo . ambapo kwa taarifa za wazazi wake mtoto huyo aliwahishwa hospitari na hali yake inaendelea vizuri
 Evarist martin mpendakura ni mwenyekiti wa kata ya senga amesema idadi ya makazi yapatayo 12 yameathiriwa na mvua hiyo iliyo nyesha siku ya tarehe16.11.2015

miaongoni mwakaya zilizo athirika ni pamoja na kaya ya emannuel longino, laulent ismail, peter martin,renatus kauzen, enrick mikoma, raimund sundi,

 wengine ni martin kauzen,filbeth kalinji, odrik kawelela, dismas kauzen, isaya kawelela na robert mikoma.


 aidha amewataka wakazi wa kata hiyo kuchukua tahadhari kwa kupanda miti na kuepuka kujenga maeneo ya mabondeni ili kuepuka kukumbwa na majanga haya yatokanayo na mvua kubwa zinazoendelea kunyesha hukuzikiwaacha wananchi katika hali ya uduni wa maisha
ameongeza kwa kuitaka pia serikari kuhakikisha wanashughurikia mapema na kulipatia ufumbuzi tatizo hili lililowakumba wananchi hususani walio kosa makazi kutokana na janga hilo
 kwa hatua nyingine mvua hiyo iliweza kuharibu
pia paa la maabara ya shule ya sekondari mbizi
iliyopo kata ya SENGA Manispaa ya sumbawanga mjini

ambapo mwalimu mkuu wa shule hiyo bi. pudensiana john kambole ,amesema mvua hiyo iliyoandamana na upepo mkali ulivuma na kupezua paa la maabara hiyo pamoja na mbao ambapo mabati yapatayo nane kuezuliwa.













kata hii ya Senga iliyopo wilayani sumbawanga mkoani rukwa ni kata  yenye wakazi wapatao 6,793 kwa takwimu ya mwaka2012 ,  ambayo idadi kubwa ni wakulima na wafugaji

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot