ZIWA RUKWA MBIONI KUPOTEA - MAISHA ONLINE BLOG

Hot

Post Top Ad

Your Ad Spot

Tuesday, April 12, 2016

ZIWA RUKWA MBIONI KUPOTEA

SERIKALI  MKOANI RUKWA IMETAKIWA  KULINDA  VYANZO VYA MALIASILI ZILIZOPO KWA  LENGO LA  KUKABILIANA NA CHANGAMOTO ZINAZO ATHIRI UCHUMI UTOKANAO NA VYANZO HIVYO ILI KULETA MAENDELEA YA MKOA NA TAIFA KWA UJUMLA

AKIZUNGUMZA   NA KITUO HIKI MWENYEKITI WA TAASISI YA JUKWAA LA MAENDELEO MKOANI RUKWA BI JOSEPHA MICHESE  AMESEMA  KUWA  VIPO VYANZO MBALIMBALI VYA  MALIASILI VINAVYO ATHIRIWA KUTOKANA NA SHUGHULI ZA KILA SIKU ZINAZOFANYWA NA  WAKAZI WANAOZUNGUKA VYANZO HIVYO IKIWEMO UVUVI HARAMU, UFUGAJI  NA UKATAJI MITI OVYO

AMESEMA  ZIWA RUKWA NI CHANZO  MUHIMU  SANA CHA MALIASILI  KINACHO LIINGIZIA PATO MKOA  NA TAIFA  AMBACHO KWA SASA  KINAENDELEA  KUKUMBWA NA SHUGHULI  ZA KILA SIKU ZA ZINAZOFANYWA NA WANAJAMII KWA   KUTOA SAMAKI AMBAO  HAWAJAFIKIA KIWANGO CHA KUVUNWA  HALI ITAKAYO SABABISHA KUPOTEA  KWA ZIWA HILO KWA KISINGIZIO CHA MABADILIKO YA TABIA NCHI.

NAE HAMIS ISA KIDEVU  AMBAE NI MUHAMASISHAJI  KATIKA ASASI YA VIJANA INAYOSHUGHULIKA NA  MASUALA YA UTUNZAJI WA MAZINGIRA MKOANI RUKWA  AMESEMA PAMOJA NA   JITIHADA ZA SERIKALI  KUENDELEA  KUPAMBANA NA KUZUIA SHUGHULI HARAMU ZINAZOFANYWA KATIKA ZIWA HILO   BADO   SHUGHULI ZA UKATAJI WA MITI NA UTUNZAJI OVYO WA MAZINGIRA ZINAENDELEA

  TUNAPOZUNGUMZIA ZIWA  RUKWA  TUNAMAANISHA PIA UHAI WA HIFADHI  ZINAZOLIZUNGUKA ZIWA HILO PAMOJA NA KUWEPO KWA   SAMAKI KAMA Kambale, Kachinga, Magege na wengine wengi wanaofaa kwa kitoweo pia  lina samaki wa mapambo ambao ni kivutio kingine cha watalii kutoka ndani na nje ya nchi.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot