WANANCHI
wa Kijiji cha Ikaka A, Kata ya Ikaka Wilayani
Mpanda Mkoani Katavi wameiomba serikali
kusajiri shule iliyoanzishwa kwa
nguvu za wananchi pamoja na kutatua changamoto za kielimu zinazowakabili kijijini
hapo.
wakizungumza na waandishi wa habari,WANANCHI hao wamesema kuwa watoto wao wanakosa elimu
bora kutokana na kutokuwa na shule inayotambulika kwa huduma ya elimu.
Mmoja
wa walimu wanaofundisha katika shule hiyo Bw.Magembe Ekingo amesema shule hiyo ina
Jumla ya wanafunzi 180 ambapo idadi hiyo inajumuisha wanafunzi wa darasa la
kwanza hadi la tatu.
Bw
Magembe ameongeza kuwa shule hiyo ambayo imejengwa kwa nyasi, ina choo kimoja huku wanafunzi wakikalia matofali jambo ambalo linarudisha nyuma maendeleo ya elimu
kijijini hapo.
Kwa
upande wake mwenyekiti wa kijiji hicho Bw.Ngoko Eliasi amesema serikali ya
kijiji hicho imeweka mkakati wa kila kaya kuchangia shilingi elfu 40 kwa ajili ya ujenzi wa shule hiyo.
Maeneo
mengine ambayo kwa sasa hayana shule maalumu inayotambulika na serikali kwa
ajili ya watoto kusoma ni pamoja na Kijiji cha Luhafwe kilichopo Kata ya Mpanda
Ndogo iliyopo Wilayani Mpanda ambapo eneo hilo ndilo lililoathiriwa na
Oparesheni Tokomeza ujangili mwaka 2013 ikisemekana kuwa eneo hilo ni hifadhi.
No comments:
Post a Comment