majaliwa:dawa nafedha zitumike Kwa malengo sahihi kati kwenye maduka Ya serikari - MAISHA ONLINE BLOG

Hot

Post Top Ad

Your Ad Spot

Tuesday, January 17, 2017

majaliwa:dawa nafedha zitumike Kwa malengo sahihi kati kwenye maduka Ya serikari


WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA  Aziagiza wizara za afya chini
WAZIRI Mkuu wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Mh.Kassim Majaliwa ameziagiza Wizara za Afya maendeleo ya Jamii Jinsia wazee na watoto pamoja na Wizara ya fedha kusimamia maduka ya serikali yanayojengwa katika hospitali za serikali ili kuhakikisha dawa na fedha zinatumika katika maelengo yaliyokusudiwa.
Waziri Mkuu ametoa agizo hilo leo wakati akizindua duka la dawa la Mkoa wa Katavi ambalo limejengwa na Bohari a Dawa Tanzania MSD katika hospitali ya Wilaya ya Mpanda.
Aidha Waziri Mkuu amesema serikali imetenga jumla ya Shilingi Bilioni 251 ili kununua dawa zitaazotumika katika hospitali zote hapa nchini.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Bohari ya dawa nchini MSD Laurean Rugambwa Bwanakunu amesema duka la dawa Mkoani Katavi lililogharimu Shilingi milioni 55 na kwa sasa likiwa na dawa zenye thamani ya Shilingi Milioni 104 litakuwa likitoa huduma vituo 580 vya huduma za afya katika Mikoa ya Katavi,Kigoma na Tabora vikiwemo 11 vya Mkoa wa Katvi.
Katika hatua nyingine Mkoa wa Katavi umepewa Shilingi Bilioni 1.5 kwa ajili ya kuanza ujenzi wa Hospitali ya Mkoa ili kupunguza msongamano mkubwa wa wagonjwa katika Hospitali ya Wilaya ya Wilaya ya Mpanda inayotoa huduma mkoa wa mzima.
Uzinduzi wa duka la dawa katika hospitali ya Wilaya ya Mpanda ni utekekelzaji wa ahadi ya serikali iliyoitoa mwaka jana kwa wakazi wa Mkoa wa Katavi ikisema kuwa itajenga Bohari ya dawa mkoani Katavi.
Waziri Mkuu pia alikuwa ameambatana na viongozi mbalimbali ktoka wizarani akiwemo Waziri wa Nishati na Madini Mh.Profesa Sospeter Muhongo pamoja na  Naibu waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhandisi Isack Kamwelwe.
     

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot