AUAWA NA KUTUPWA MTONI, MKOANI RUKWA KIJIJI CHA SAKALILO KATA YA ILEMBA - MAISHA ONLINE BLOG

Hot

Post Top Ad

Your Ad Spot

Tuesday, January 17, 2017

AUAWA NA KUTUPWA MTONI, MKOANI RUKWA KIJIJI CHA SAKALILO KATA YA ILEMBA



 Kijana mmoja 44, Mkazi wa Sakalilo kata ya ilemba,ameuawa kwa kukatwa na kitu chenye ncha kali kichwani kisogoni na kisha kutupwa chini ya daraja  la mto Mumba na watu wasiojulikana.

 

marehemu  huyo aliye julikana kwa jina la KALTUS JACOB,ni mfipa na ni mkazi wa kijiji cha sakalilo kata ya ilemba tarafa a kipeta wilaya ya laela mkoani Rukwa.
 
Aidha kabla ya tukio marehemu alionekana akiwa kilabuni na wake zake wawili wakinywa pombe na aliwaaga na kuondoka na hakurudi tena hadi alipokutwa akiwa amefariki.


Chanzo cha mauaji hakijajulikana juhudi za Jeshi la Polisi zinaendelea ili kubaini kiini cha mauaji hayo.

Mwili wa marehemu umekabidhiwa kwa ndugu zake kwa ajili ya mazishi mara baada ya kufanyiwa uchunguzi wa kidaktari na kugundua kuwa alichomwa na kitu chenye ncha kali na kutupwa mtoni.
Watuhumiwa hawajakamatwa na uchunguzi unaendelea ili kuweza kuwabaini waliohusika katika mauaji hayo.
                                                     
 Kamanda wa Polisi Mkoa wa Rukwa Kamishna Msaidizi wa Polisi GEORGE SIMBA KYANDO ametoa wito  kwa wananchi  kuwa atalifuatilia suala hilo na atahakikisha wamekamatwa na kufikishwa katika vyombo vya sheria kwa hatua zaidi. 

Aidha anatoa ushauri kwa wananchi waweze kushirikiana na Jeshi la Polisi kwa kutoa taarifa katika vituo vya Polisi vilivyo karibu nao ili kuweza kurahisisha kazi ya kupambana na wahalifu na kuzuia uhalifu.


No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot