SERIKALI YATAKIWA KUTOA ELIMU YA KUTOSHA JUU YA UMILIKI ARDHI KWA WAKULIMA WADOGO :SUMBAWANGA - MAISHA ONLINE BLOG

Hot

Post Top Ad

Your Ad Spot

Tuesday, March 15, 2016

SERIKALI YATAKIWA KUTOA ELIMU YA KUTOSHA JUU YA UMILIKI ARDHI KWA WAKULIMA WADOGO :SUMBAWANGA


 serikari imetakiwa kutoa elimu ya kutosha juu ya sheria ya umiliki wa ardhi  kwa lengo la kuifanya jamii ya wakulima kutambua haki msingi ili kuepukana na migogoro inayoweza epukika na kumfanya mkulima kunufaika na shughuri za kilimo

wakizungumza katika mkutano ulioandaliwa na asasi inayoshughurika na kuwezesha mchakato wa upatikanaji na udhibiti wa ardhi bora kwa wakulima wadogo(MIICO)  wamesema kuwa elimu juu ya hati miliki ni msingi kwa wananchi kwani bila elimu hiyo mwananchi hatokuwa na sauti katika kuitetea na kulinda ardhi ,

 katika mkutano huo baadhi ya wajumbe wametoa tafakari ya pamoja ,katika kuwawezesha wakulima wadogo kwa kutoa mikakati mbalimbali ikiwa ni pamoja na serikali kuwahakikishia wakulima wadogo hati miliki ya ardhi, kabla ya kuwaruhusu wawekezaji wakubwa


MIICO NI asasi ya serikari iliyosajiliwa na serikari mwaka 2005 yenye lengo la kujenga uelewa wa pamoja juu ya lengo la mradi wa upatikanaji wa ardhi kwa wakulima wadogo ambapo kwa mkoa wa rukwa asasi hii inafanya kazi na kata nne ikiwa ni pamoja na kata ya kanda,sandulula, msanda muungano na mpwapwa

aidha viongozi mbalimbali waalio hudhuria ni pamoja,mwenyekiti wa halmashauri,DAS -ofisi ya mkuu wa wilaya, afisa ardhi-kaimu mkurugenzi, afisa maendeleo ya jamii, madiwani kata ya kanda, sandulula,msanda muungano, kanda na mpwapwa, wenye viti wa kijiji toka kata husika, mkurugenzi wa KAESO.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot